Kamanda wa Operesheni Kanda Maalum Dar es Salaam Lucas Mkondya amesema, watuhumiwa hao walikamatwa Juni 12, saa 2 asubuhi maeneo ya Ubungo National Housing ambapo walipelekwa kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mansor Bakari, Mjuli Jeremia ,Edger Mrope, Daniel Rogasian ambao baada ya uchunguzi watapelekwa mahakamani.
Amesema kuwa katika tukio lingine Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja Emmanuel Dickson katika eneo la Vingunguti akiwa na bastola aina ya Signature ambapo alianza kufyetua risasi kabla ya kupigwa risasi ya mguuni na polisi lakini alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikopelekwa kwa ajili ya matibabu
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kukamata risasi 117 za bunduki aina ya SMG katika eneo la Mbagala Kilungule ambazo zilikuwa zimebebwa na Abilah Rashid katika mfuko.