Tuesday , 2nd Aug , 2016

Wakazi wa vijijini vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya Mkomanzi wilayani Same,mkoani Kilimanjaro vinakabiliwa na uhaba wa Maji safi na Salama, kutokana na wanyama kuharibu miundombinu ya Maji.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi

Wakizungumzia Changamoto hiyo wakazi hao wamesema kuwa wakati wa Kiangazi baadhi ya wanyama wamekua wakiaharibu miundombinu ya miradi ya maji hivyo kuwafanya kutembelea umbali mrefu kutafuta maji.

Wakazi hao wa vijiji vya Mkirani, Maole, Kadando na Muheza, wamesema kuwa hali inawafanya kuhatarisha maisha yao na pia kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi na maendeleo kutokana na kuhofia wanyama wakali katika hifadhi hiyo.

Kufutias uwepo wa Changamoto hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya TANAPA, Allan Kijazi, amesema kuwa itashughulikia tatizo hilo kwa kukarabati miundombinu ya maji iliyoharibiwa na wanyama hao.