Mmoja wa wanafunzi aliyejeruhiwa kutokana na hofu ya tukio la ugaidi baada ya kutokea mlipuko wa transfoma katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kampasi yake ya Nakuru.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa kumi alfajiri limetokea katika kampasi ya Kikuyu, na kuibua hofu na hali ya taharuki baada ya wanafunzi wengi kudhani mlipuko huo ni tukio la kigaidi.
Hali hiyo ilipelekea wanafunzi hao kuruka kutoka juu ya ghorofa wengine hadi kutokea ghorofa ya sita ya hosteli yao katika kujaribu kujinusuru, ambapo wengi wao wamejeruhiwa vibaya.
Wanafunzi wapatao 100, wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Kenyatta, na wengine wamepelekwa hospitali za Mtakatifu Teresa na Karen.
Taharuki ya leo imetokea takribani juma moja baada ya tukio baya la kigaidi kutokea katika Chuo Kikuu cha Garissa huko kaskazini mashariki mwa Kenya, ambapo wapiganaji wa kundi la Kigaidi la Al-Shabaab la nchini Somalia kuvamia na kuwauwa wanafunzi 148 chuoni hapo.