Tuesday , 16th Feb , 2016

Zaidi ya wakazi 5000 wa kata ya Laroi wilaya ya Arumeru Magharibi Mkoani Arusha wanakabiliwa na adhaa kubwa ya ukosefu wa barabara na vivuko,jambo linalohatarisha maisha yao kwa kukosa huduma za muhimu za kibinaadamu hasa kipindi cha mvua.

Diwani wa kata Laroi wilaya ya Arumeru Magharibi Mkoani Arusha Ojungu Salekwa.

Wakiongea na East Africa radio baadhi ya wakazi hao wamesema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitaabika huku hali ikiwa mbaya zaidi kwa wakinamama wajawazito na watoto pale wanapohitaji huduma za dharurula huku wakibainisha hali hiyo imeanza tangu uhuru.

Aidha wakazi hao wameongeza kuwa kundi linguine linalo taabika na ukisefu wa barabara za ukakika katika kipindi chote cha mwaka ni wanafunzi wa shule ya sekondari Oljoro ambao hulazimika kuomba hifadhi kwa watu waliojirani na shule hiyo.

Kufuatia malalamiko hayo diwani wa kata hiyo Ojungu Salekwa, juu utatuzi wa tatizo hilo na amesema kuwa hatua alizozichukua ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kulishughulikia.