Wednesday , 6th Jul , 2016

Wajasiriamali wadogo nchini wametakiwa kutengeneza bidhaa zao kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na mamlaka husika ili kuweza kumudu ushindani wa soko.

Wajasiriamali wadogo nchini wametakiwa kutengeneza bidhaa zao kwakuzingatia viwango vilivyowekwa na mamlaka husika ili kuweza kumudu ushindani wa soko.

Mkurugenzi wa mradi wa ubunifu katika masuala ya kijinsia na kuhimarisha chakula katika ngazi ya kaya nchini Rozi Kingamkono ameyasema hayo wakati akizungumza na wajasiriamali kuhusu namna yakuwapatia ujuzi na kuboresha masoko yao ya mitaji sambamba na kuhimarisha biashara zao.

Amesema mradi huo umelenga kuwasaidia wanawake na wajasiriamali wadogo waweze kufanya shughuli zao kwa njia rahisi yakutumia mashine za kisasa, kwakuwa kundi hilo kubwa ndio linalozalisha chakula kwa wingi nchini.

Bi.Kingamkono amesema njia ambazo zinatumika kwa sasa katika uzalishaji wa chakula hazitoshelezi kutoa mahitaji na ubora wa vyakula hivyo kwakuwa wanatumia muda mwingi na kuna wakati wanaathirika kiafya kutokana na kufanya shughuli hizo kwakutumia Tekinolojia ya zamani.

Kwa upande wao wajasiliamali hao wamesema kutokana na kukuwa kwa Tekinolojia duniani ni wajibu kwa taifa kufikiria zaidi katika kutoa elimu ya ujasiriamali wa kisasa ili kuwawezesha kuongeza mapato yao na pato la taifa kwa ujumla.