
Waziri Mkuu akijumuika na waisilamu wengine katika swala ya Eid, leo
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa swala ya Eid El Hajj , katika viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, waziri Majaliwa amesema yeyote mwenye uwezo ajitokeza kuwasaidia wahanga hao ili waweze kurudi katika shughuli zao za maendeleo za kila siku.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka waislam kote nchini kuendelea na kusisitiza uwepo wa amani nchini ili kila mtanzania atimie majukumu yake kwa amani na utulivu.
Aidha Majaliwa ameongeza kuwa serikali nayo kwa upande wake itaendelea kudumisha amani na kumfanya kila mtanzania aweze kuabudu kwa uhuru na amani na kurithisha vizazi vijavyo hali ya utulivu iliyopo sasa.
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA limefanya mabadiliko mapya ya kimfumo katika uboreshaji wa utoaji elimu ya dini hiyo ambapo sasa waislamu watafundishwa elimu ya taaluma mbalimbali tofauti na hapo nyuma ambapo walifundisha elimu ya dini pekee.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheihk Abubakary Zubery Bin. Ally amesema hayo leo wakati akiongoza mamia ya waumini wa kiislamu katika baraza kuu la Iddi lililofanyika leo jijini Dar es Salaam Makao makuu ya Baraza hilo.
Mufti Mkuu amewataka waislamu na watanzania kwa ujumla kutunza amani ya nchini na kutoadaika na baadhi ya watu kutoka nje au ndani ya nchi wasio litakia mema taifa letu na kuwalaghai ili wavunje amani.