Wednesday , 6th Jul , 2016

Wakati waumini wa Dini ya Kiislamu nchini wakiungana na wenzao ulimwenguni kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitri wito umetolewa kwa waumini hao kuendelea kuienzi na kudumisha amani iliyopo nchini.

Wito huo umetolewa leo na Mwalimu wa Dini ya Kiislamu katika Madrasa ya Msikiti Mkuu wa Mbeya, USTADHI KHERY KATANGA wakati akizungumza na East Afrika Redio.

Ustadhi KATANGA amesema waumini wa Kiislamun na watanzania kwa ujumla wanapaswa kusherehekea sikukuu ya Eid kwa amani na kuepuka kufanya maovu kama alivyoagiza Mtume Mohamed.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuwa waangalifu na watoto wao wakati wa sherehe hii kwani wanaweza kupatwa na hatari ya kubakwa au kulawitiwa na watu wenye nia ovu.

Ustadhi Khery Katanga