Monday , 1st Dec , 2014

Serikali  imesisitiza  kuwa   haitakuwa  na  msamaha   kwa   viongozi   na  watendaji   ambao   wametajwa    kwa   namna   moja   au  nyingine kushiriki   katika  uchotwaji   wa  mabilioni   ya  fedha  katika  akaunti   ya  Tegeta  Escrow

Serikali  imesisitiza  kuwa   haitakuwa  na  msamaha   kwa   viongozi   na  watendaji   ambao   wametajwa    kwa   namna   moja   au  nyingine kushiriki   katika  uchotwaji   wa  mabilioni   ya  fedha  katika  akaunti   ya  Tegeta  Escrow   kitendo  ambacho   kimesababisha   serikali  kupoteza  mabilioni   ya  fedha  kama  kodi.
 
Naibu   Waziri  wa  fedha Mh   Mwigulu  Nchemba  ambaye   pia   ni   Naibu  Katibu   Mkuu  wa  CCM   Tanzania  Bara,   amesema  hayo  mjini  Musoma  wakati  akihutubia mkutano wa hadhara   baada  ya  kuwaapisha  makamanda   na  manaibu   makamanda   wa  umoja  wa  vijana  wa  CCM   wilaya  na  mkoa  wa  Mara, ambapo   amesema  lazima   hatua  kali    za   kinidhamu, kimaadili  na  kisheria   zichukuliwe    kwa   wahusika   wote    kama  ilivyoazimiwa  na  bunge la  jamhri   ya  muungano  wa  Tanzania.
 
Hata  hivyo  Naibu  huyo   Waziri wa Fedha amekiri  kuwa  katika   zoezi   la  ubinafsishaji   wa mashirika   ya  umma hasa   katika  sekta  ya  viwanda  serikali  ilifanya  makosa  makubwa  katika zoezi   hilo  kwa  kuwapa   watu  ambao   wengi   wao  wamekiuka  mikataba  ya  uendeshaji   wa viwanda  hivyo  hatua  ambayo  imesababisha   viwanda  vingi kushindwa kufanya  kazi   na  kufanya  vijana  wengi  sasa  kukosa  ajira  huku  serikali  ikikosa  kodi  kupitia  viwanda  hivyo.
 
Kwa  upande   wake  mjumbe  wa  halmashauri  kuu  ya  taifa   wa   Chama  Cha  Mapinduzi  Vedastus Mathayo, ameishukuru  serikali  kwa  kukubali  kutekeleza  mradi  wa  maji wenye  thamani  ya  zaidi  ya  bilioni  50   ambao   amesema  kukamilika  kwake   kutaondoa  kabisa  tatizo   la  maji   kwa   manispaa   ya  Musoma  pamoja   na  kukubali  kugharimia  ujenzi  wa  hospitali  ya  rufaa  ya  mkoa  wa  Mara  katika  eneo  la  Kwangwa