Monday , 28th Nov , 2016

Taasisi ya wahandisi Tanzania imeiomba serikali kuweka Mhadisi Mkuu wa Serikali ambaye ataratibu na kusimamia sekta zote za uhandisi nchini ili kuongeza ufanisi na kukuza taaluma hiyo yenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya teknolojia nchini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilia

Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano la 10 la kimataifa la Wahandisi, Rais wa Taasisi hiyo Mhandisi Prof. Joseph Runyoro, amesema kutokuwepo kwa Mhandisi Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa mambo yanayokwamisha tasnia hiyo kutokana na kukosa ngazi ya juu ya maamuzi na usimamizi wao nchini.

Aidha, Rais huyo amewataka waandisi kote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia malengo endelevu ya dunia ili kuchochea mapinduzi ya viwanda na kusogeza pato la taifa kufikia uchumi wa kati.

Ili kuleta mapinduzi ya kutosha, Taasisi ya Waandisi Tanzania imeandaa kongamano kwa kushirikiana na jumuiya ya taasisi za kihandisi ya Afrika ya Mashariki itakayo fanyika mkoani Arusha ili kuangazia namna ambavyo wanaweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia malengo endelevu.