Thursday , 31st Mar , 2016

Idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro wamefanikiwa kukamata wahamiaji haramu 11 raia wa Ethiopia kwa nyakati tofauti wakati wakijiandaa kusafirishwa kuelekea nchi za kusini mwa Tanzania.

Wahamiaji haramu

Idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro wamefanikiwa kukamata wahamiaji haramu 11 raia wa Ethiopia kwa nyakati tofauti wakati wakijiandaa kusafirishwa kuelekea nchi za kusini mwa Tanzania.

Akitoa taarifa ya kukamatwa wahamiaji hao Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mkoa Morogoro Joseph Malumbu, amesema wahamiaji hao walikamatwa katika maeneo ya kituo cha mabasi Msamvu, wawili wamekamatwa katikati ya mji na wengine saba katika eneo la Sangasanga Mzumbe.

Kamishna Malumbu amesema kuwa Morogoro sasa sio mahala pa kupitisha wahamiaji bali wataendelea kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahamiaji wote watakaogundulika mkoani hapo.

Kufuatia kukithiri kwa matukio ya kukamatwa wahamiaji haramu katika mkoani Morogoro na maendeo mengine baadhi ya wakazi wa mji wa huo wameshauri wananchi wanaoishi katika mikoa ya mipakani kutoa taarifa ya watu wasiowajua kwenye vyombo vya usalama ili wachunguzwe na kuchukuliwa hatua madhubuti.

Hata hivyo mkoa wa Morogoro umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya wahamiaji haramu mara kwa mara hili inayotishia usalama wa mkoa hivyo ipo haja wa serikali kuona umuhimu wa wa kuimarisha ulinzi wa mipaka katika mikoa iliyopo pembezoni ili wananchi na mali zao waweze kuishi kwa usalama.