Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akibadilishana mawazo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani.
Sheikh Shaaban ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ibada ya Eid el Fitri kwenye msikiti wa Ghaddaf uliopo mjini Dodoma.
Amesema kuna baadhi ya waandishi wa habari ambao wamekuwa wakitoa taarifa za uongo ili kuchafua watu au taasisi flani baada ya kupokea rushwa kutoka kwa watu wanaotaka kuwachafua wenzao.
Amesema hata vitabu vya dini vimekataza kutoa hukumu kwa upande mmoja wa mashtaka na kuwataka waandishi wa habari kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili yao katika kutekeleza majukumu yao ya kuipasha jamii habari kwa kuwa inawaamini.