Baadhi ya wajumbe wa chama cha wafanyakazi serikali kuu na afya (TUGHE) wakiwa katika moja ya mikutano yao.
Katibu wa chama cha wafanyakazi serikali kuu na afya(TUGHE)mkoa wa Iringa Shadrack Mkodo amesema kuwa suala hilo limekuwa changamoto kwa waajiri wengi kutokana na kuwa waajiri wengi wanafanya kazi kwa mazoea.
Amesema kuwa waajiri wengi hawataki kuanzisha mabaraza ya wafanyakazi mahali pa kazi jambo ambalo ni takwa la kisheria na kwa kufanya hivyo wanakuwa kinyume na sheria kutokana na kuwa sheria inawataka kufanya hivyo.
Aidha katibu huyo amewataka wafanyakazi kuacha kutoa lugha chafu kwa wateja wao na kufuata taratibu na sheria za kazi kwa weledi wa hari ya juu.
Hata hivyo katibu ameongeza kwa kusema kuwa kwa mujibu wa sheria katika kifungu cha nane kinasema kuwa kwa yoyote atakayetoa lugha chafu atapewa onyo, kushushwa cheo na hata kufukuzwa kazi.