
ACP Abwao ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa, ni mwendo kasi wa dereva wa Hiace iliyokuwa na abiria ikitokea Kakola kwenda Kahama mjini, na kwamba barabara hiyo imekuwa na vumbi nyingi.
''Barabara ya Kakola, Kahama imekuwa na vumbi nyingi, kwasababu imekuwa ikitumiwa na magari mengi hii ni baada ya kuibuka kwa machimbo mapya ya Kakola Namba 9'' amesema ACP Abwao.
Aidha Kamanda Abwao amesema, baadaye leo atatoa taarifa rasmi za ajali hiyo, ikiwemo majina sahihi ya watu waliopoteza maisha na majeruhi wa ajali hiyo.