
Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Mbeya Bw. Haji Mnasi alipotembelea kaburi la Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililopo Wilayani Butiama Mkoani Mara kwa lengo la kujifunza baadhi ya mambo aliyokuwa akiyafanya baba wa taifa na kusisitiza uwajibikaji, uzalendo, uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania.
Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hayo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kwa kuwatumikia wananchi.
Amesema kupitia kumbukumbu za Mwl.Nyerere watumishi wajifunze ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika, kwakua wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine.
Kwa upande wake Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw. Jacob Thomas amesema kuwa watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika makumbusho hiyo.
Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.