Monday , 4th Apr , 2016

Vijana wametakiwa kuacha kulalamika suala la ajira kuwa ni tatizo na badala yake watumie fursa mbalimbali zilizopo nchini hasa katika sekta ya kilimo ili kujiajiri wenyewe na kujikomboa kiuchumi.

Vijana wakiwa katika uendelezaji wa Kilimo cha Vitunguu

Wito huo umetolewa na mratibu wa sera kutoka chuo cha uhasibu Arusha, Khamis Mwande wakati wa Kongamano la vijana la kuonesha uwezo wao kitaaluma katika kutafuta fursa za ajira.

Mwande amesema kuwa endapo vijana watajikita kwenye kilimo hasa cha mbogamboga ambacho kinakuwa kwa kasi na soko lake ni kubwa ndani na nje ya nchi hivyo hakuna sababu ya kijana kuogopa kujishughulisha na kilimo.

Mwande amesema kuwa vijana wanapaswa kuondokana na dhana kuwa kilimo ni kwa ajili ya wazee peke yake katika kujiingia kipato cha kila siku hivyo ni wajibu wao sasa kujiingiza katika kilimo ambacho kina uwanja mpaka wa kibiashara.

Vijana hao wa chuo cha Uhasibu wamekutana siku ya ugunduzi wa vitu ambavyo vinaweza kuwapatia fursa ya kupata ajira nchini kwa kufanhya maonyesho kwa wadau mbalimbali ambao wana fursa za ajira.

Kwa upande wake Meneja wa Utetezi kutoka taasisi ya TAHA, Kelvin Remi amesema ni vyema vijana wanapomalizia masomo yao wakajikita katika kilimo cha mbogamboga ambacho hakihitaji eneo kubwa na mtaji mkubwa.

Sauti ya mratibu wa sera kutoka chuo cha uhasibu Arusha, Khamis Mwande akiongelea fursa kwa vijana