Saturday , 18th Apr , 2015

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa CCM, (UWT) Mkoa wa Arusha Flora Zelote amewatahadharisha viongozi wa kitaifa wa CCM, kurejesha majina yale yale ya wagombea, watakayoyapendekeza vinginevyo,tofauti watakuja kuwanadi wao katika kampeni.

Wanachama wa UWT Jimbo la Arusha mjini wakimshangiria Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (pichani hayupo katika mkutano wa mwisho wa ndani wa CCM.

Zelote ametoa angalizo hilo jana, alipokua akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uhai wa jumuiya na chama, katika kata mbalimbali za wilaya ya Arusha.

Amesema hali ilivyo sasa chama kinapaswa kuheshimu matakwa ya wananchi ya nani wanamtaka, badala ya kuendelea na tabia ya kuwapendekeza watu kwa utashi wa kikundi cha watu, jambo ambalo linasababisha ugumu katika kuwanadi wagombea hao.

Amesisitiza kuwa msimamo wa jumuiya hiyo mkoa wa Arusha, kutowafanyia kampeni wagombea watakaopatikana kwa utashi wa viongozi badala ya wananchi na watakaa pembeni..

Amesema maamuzi hayo pia yatafuatwa katika ngazi ya mkoa na wilaya vilevile, pindi watakapoacha mapendekezo ya kata zao na wilaya zao, wakafanya vinginevyo nao watapewa taarifa, kuja kuwanadi wagombea wao waliowarejesha kwa utashi wao.