Sunday , 31st Jan , 2016

Mtayarishaji wa Muziki wa Muda mrefu nchini Tanzania Master Jay amesema mfumo wa kidigital ndiyo ulioua soko la albam nchini na ndicho kilichowafanya wasambazaji wengi waachane na biashara hiyo kwa kuwa hailipi.

Mtayarishaji wa Muziki wa Muda mrefu nchini Tanzania Master Jay

Master Jay amefunguka zaidi na kusema kuwa sasa ivi msanii akitoa ngoma tu haichukui dakika inakua imesambaa nchi nzima huku wengine wakijinufaisha kwa mfumo huo kwa kuuza ngoma kwa bei rahisi.

Master Jay amesema wasanii wanaosema msanii lazima utoe albam ni kujidanganya kwa sababu kwa sasa mfumo wa uuzaji wa albam hauna faida kabisa kwa wasambazaji