
Naibu Waziri ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Singida Martha Mlata CCM aliyetaka kujua ni lini serikali itafanya jitihada za makusudi za kuvuta maji kutoka wilayani Igunga kwenda Singida kwa kuwa mkoa huo ni mkame maneo mengi na kukosa vyanzo vya uhakika vya maji.
Naibu Waziri Kamwele amesema kwamba pamoja na jitihada nyingine zinazoendelea katika miradi ya maji mkoa wa Singida bado serikali inamuagiza Mhandisi Mshauri wa maji mkoa wa Singida kuanza kufanyia kazi suala la kuvuta maji kutoka Igunga kwenda Singida.
Aidha Naibu Waziri Kamwele amesema wananchi wanaotoka karibu na vyanzo vya maji wataanza kupata maji kabla ya watu wengine kwenda kupatiwa maji katika maeneo mengine.
Mhandisi Kamwele ameyasema hayo kufuatia eneo la Mwangoko kuwa na chanzo cha majib ambayo yatatumika na wananchi wa Singida hivyo waliopo katika chanzo hicho watapewa kipaumbele