Friday , 14th Aug , 2015

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernad Membe amesisitiza Watanzania waishio Ughaibuni(Diaspora),kuwa na uraia pacha kwa kuwa ndio njia pekee ya ushirikiano wa kiwekezaji na kukuza uchumi wa nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe

Waziri Membe ameongea hayo katika mkuu wa pili wa wanadiaspora nchini wenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya watanzania waishio nje na wale wafabiashara wadogo na wakubwa nchini Tanzania.

Membe amesema kuwa serikali inatumia fedha nyingi kuaajri watalaamu kutoka nje ya nchi na kuwalipa fedha nyingi wakati kuna uwezekano wa kuwatumia watanzania hao waishio nje kufanya kazi nchini na kuwekeza katika kukuza uchumi wa nchi.

Membe ndio mwanzilishi wa Diaspora nchini Tanzania na anasimamia msimamo wake wa kuwa na raia Pacha ingwa kwenye katiba iliyopendekzwa suala hilo halijawekwa kwa vile alivyopendekeza.

Wakati huo huo Membe alitumiac mkutano huo kuelezea kilichotokea katika Uchaguzi wa Mgombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi na kusema ulikua ni kama mchezo uliamuliwa kwa penalti na kusema alikubali matokea kwa hatua ambayo ilifikia.