Thursday , 5th Mar , 2015

Unyanyasaji wa kijinsia haswa kwa wanawake umesababisha wanawake wengi nchini Tanzania kuwa masikini na wenye uchumi dhaifu japo wao ni wengi zaidi kuliko hata wanaume.

Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi katika Halfa ya kuelekea katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia katika viwanja vya TGNP Dar es salaam.

Bibi Liundi amesema kuwa Mfumo dume umekuwa ukiwaweka kando wanawake katika Miradi ya Uzalishaji mali na uchumi kwa ujumla na hivyo kusababisha wanawake wengi kuwa masikini hasa vijijini na kuwa wasindikizaji tu wa Maendeleo ya wanaume.

Kwa upande wa washiriki wao wamesema sasa ni zamu ya wanawake sasa kuinuka kiuchumi nakuitaka Serikali kuwasaidia hasa maeneo ya kupata Ajira na Mikopo kwa wanawake haswa vijijini.