Friday , 28th Nov , 2014

Shirika la umoja wa mataifa linalohudumia watoto la UNICEF limesema kuwa lipo tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania kujenga mahakama ya watoto mkoani Mbeya kwa lengo la kuhudumia watoto wanaokinzana na sheria nchini.

Mtaalam wa ulinzi na usalama wa mtoto wa shirika la UNICEF nchini Tanzania Mbelwa Gabagumbi.

Mtaalam wa ulinzi na usalama wa mtoto wa shirika la UNICEF nchini Tanzania Mbelwa Gabagumbi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango wa marekebisho ya tabia na mpango wa utoaji wa msaada wa sheria kwa watoto wanaokinzana na sheria nchini ambao umefanyika jijini Mbeya.

Kamishna msaidizi kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Babikira Mushi amesema uamuzi wa kujenga mahakama hiyo Mbeya umefikiwa baada ya kubaini kuwa mkoa huo una vigezo vyote vinavyostahili kwa ajili ya uanzishwaji wa mahakama ya watoto.

Baadhi ya wadau wanaohudumia watoto wanaokinzana na sheria mkoani Mbeya wamesema kuwa mazingira ya utekelezaji wa sheria ya mtoto nchini bado ni magumu kuwezesha watoto wanaokinzana na sheria kupata haki kwa mujibu wa sheria hiyo