Tuesday , 16th Feb , 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Rwanda limeelezea wasiwasi wake baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza uamuzi wa kuhamishia wakimbizi wote wa Burundi kwenye nchi zingine.

Rais Paul Kagame wa Rwanda

Idadi ya wakimbizi wa Burundi waliosaka hifadhi nchini Rwanda imefika zaidi ya 70,000, huku wakimbizi wengine 75,000 wakiwa wamekimbilia Rwanda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Ofisa wa mawasiliano wa UNHCR Rwanda, Martina Pomeroy, amesema kwamba tayari tangazo hilo limezua hofu miongoni mwa wakimbizi, akisema kwamba wizara ya masuala ya wakimbizi imehakikisha kwamba wakimbizi hawatafukuzwa mara moja na kwamba mpaka hautafungwa.

"Hakuna maelezo kuhusu muda wa kutekelezwa mpango huu, ni akina nao hao wadau wa kimataifa wanaogusiwa, hao wakimbizi wataenda nchi gani. Tunatumai kuwa serikali itatoa ufafanuzi zaidi ili kutoa hakikisho kwa wakimbizi kuwa wateendelea kupata hifadhi nchini Rwanda kwa mujibu wa kanuni za kimataifa."