Wednesday , 28th May , 2014

Taasisi ya Chakula na Lishe nchini Tanzania imesema zaidi ya asilimia 60 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano hapa nchini wanafariki kutokana na ukosefu wa lishe bora.

Maziwa ya mama ni moja ya chanzo kikuu cha lishe bora kwa watoto wachanga. Unyonyeshaji husaidia kupunguza vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Hayo yameelezwa Jijini Dar-es-Salaam na Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya lishe kutoka taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dk. Joseline Kaganda wakati alipokuwa akizungumza na East Africa Radio kuhusu tatizo la vifo vya watoto vinavyochangiwa na ukosefu wa lishe bora.

Amesema kuna baadhi ya wakina mama hapa nchini wamekuwa na imani potofu ambazo zimejengeka kwa wakina mama kwamba ukinyonyesha mtoto maziwa ya mama yanalala huku akieleza kwamba suala hilo limetokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha.