
Kigwangalla ameyasema hayo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum CCM Faida Mohamed Bakari aliyetaka kujua ni hatua gani ambazo serikali itachukua kwa kujiridhisha kwamba mzazi anakataa kutoa ushahidi juu ya kesi ya mtoto.
Dkt. Kigwangalla amesema ushirikiano wa jamii hasa katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia na matukio ya ukatili kwa watoto ni muhimu sana na utaratibu wa kuendesha kesi mahakamani ni utaratibu wa kisheria ambao unahitaji mahakama kujiridhisha kabla ya kuhukumu hivyo wazazi kutotoa ushirikiano hukwamisha kesi nyingi.
Aidha Naibu Waziri Kigwangalla amesema kwamba kesi nyingi za ukatili kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara ya afya asilimia 60 ya matukio ya ukatili hufanywa mahumbani na asilimia 56 hufanywa shuleni hivyo amewaasa wazazi kuwa makini na malezi ya watoto.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Nchemba ametoa onyo kwa wazazi na walezi watakao ficha ushahidi na ikabainika kweli wameficha juu ya ukatili wa watoto watajumuishwa kwenye uhalifu.