Monday , 14th Mar , 2016

Ugonjwa wa Kipindupindu nchini umeongezeka kutoka wagonjwa 544 wiki iliyopita hadi kufikia wagonjwa 758 wiki hii na Jumla ya watu 18,399 wameugua ugonjwa huo ambapo watu 292 wamefariki dunia na ugonjwa huo kusambaa katika Mikoa 23 nchini kote.

Kaimu Katibu Mkuu Michael John kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto nchini

Ripoti hii imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Michael John kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto nchini ambapo amesema Takwimu za Ugonjwa huo zinaonyesha mikoa ambayo tayari imeshapata Ugonjwa huo imeongezeka na kufikia Mikoa 23.

Amesema kuwa wizara hiyo imeweka mikakati zaidi ikiwa ni pamoja na kupeleka ombi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu la kutaka kuitisha mkutano wa Kamati ya Dharura ya Taifa ambayo inajumuisha Makatibu wakuu ili suala la Kipindupindi liweze kujadili kwa upana zaidi kwakuzingatia hali ya Mvua kwa sasa.

Aidha Kaimu katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau wote wa afya nchini pamoja na jamii kwa ujumla kuongeza jitihada zakuutokomeza Ugonjwa huo.