Monday , 15th Feb , 2016

Jeshi la Polisi nchini uganda linamshikilia Mgombea urais wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye .

Dkt. Kizza amekamatwa wakati akipita na gari lake mjini Jinja huku akisindikizwa na mamia ya wananchi wanaomuunga mkono ndipo polisi wakatumia mabomu ya machozi kutawanya wafuasi hao na kumkamata kiongozi huyo.

Kiongozi huyo ni mmoja wa wagombea wa urais nchini uganda ambapo uchaguzi huo unafanyika siku ya alhamisi tar 18.02.2016, ambapo Rais Yoweri Museveni nae ni miomgoni mwa wanaowania upya nafasi hiyo.

Aidha Bw Besigye alipangiwa kufanya mikutano ya kampeni leo mjini Kampala na amezuiliwa katika kituo cha Polisi Nagalama na jeshi la polisi limesema linamshikilia kwa muda na watamuachia.

Chanzo BBC