Tuesday , 15th Dec , 2015

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa 353 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo ujambazi wa kutumia silaha, wizi, Usafarishaji madawa ya kulevya na makosa mengine ya kihalifu.

Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova

Akizungumza na East Africa Radio leo Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amesema watuhuhumiwa hao wamekamatwa katika msako maalumu wa uimarishaji wa usalama wa Jiji.

Kamishna Kova ameongeza kuwa kwa sasa jeshi hilo linaendelea na operesheni hiyo maalumu ili kuhakikisha watu wanasheherekea sikukuu ya krissmass na mwaka mpya kwa amani na utulivu.

Aidha ameongeza kuwa mwishoni mwa mwaka watu wengi wanakuwa kwenye maandalizi ya kufunga mwaka lakini kuna wengine wanasheherekea kwa njia haramu ikiwemo kuvunja na kuiba.

Kova amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na kuwafanikisha kuwakamata kwa kuwa wahalafu ni wananchi wanaopatikana mtaani na wanajulikana na jamii ya watu.