Tuesday , 28th Jun , 2016

Wadau mbalimbali wa maendeo mkoani Mtwara wameendelea kuchangia madawati huku zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kufikia tarehe ya mwisho ya kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli la kutatua uhaba wa madawati nchini.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.

Jumuia ya Mpango wa Maendeleo wa Kusini Mashariki (SEDO), imekabidhi madawati 35 kati ya 60 waliyokusdia kwa Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, huku mengine wakitarajia kukabidhi wilayani Masasi kabla ya tarehe ya mwisho ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo, Dendego amesema zoezi hilo linatekelezwa vyema katika mkoa wake na kuahidi kukamilisha kabla ya Juni 30 huku akiwashukuru wadau, wananchi na viongozi wa halmashauri pamoja na wakuu wa wilaya kwa kushiriki ipasavyo katika kufanikisha jukumu hilo.

Kiongozi wa jumuia hiyo ambayo inaundwa na wanafunzi wa vyuo vikuu wa miaka ya nyuma, Dankan Bushiri, amesema madawati waliokabidhi yanathamani ya Sh. Milioni 3.5 na kuwataka wadau wengine kuguswa na suala hilo kwa masilahi ya mkoa.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.