
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania SHIVYAWATA Bi. Ummy Nderiananga amesikitishwa na kitendo cha viongozi wa serikali kutoshiriki katika ufunguzi wa wiki ya watu wasiosikia jambo ambalo limepelekea maandalizi kuwa magumu ikizingatiwa kwamba SHIVYAWATA haipokei ruzuku yoyote kutoka serikali katika kufanikisha shuguli zake
“Tumehangaika kutafuta viongozi mbalimbali kushiriki na sisi katika maadhimisho hayo lakini kila mtu hakujali na kutoa udhuru, tumehangaika kuhitaji kusafirisha viongozi wetu wa mkoa lakini bado tumeshindwa hakuna anayetuunga mkono, ndiyo sababu tukamuita Mhe. Zitto Kabwe akaja kutusaidia” amesema
Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe ametaka wawakilishi wa watu wenye ulemavu Bungeni kuchaguliwa kutokana na makundi ya watu wenye ulemavu na sio kutolewa katoka ndani ya vyama vya siasa ili kuondoa ubaguzi katika kushugulikia changamoto za walemavu.
Mhe. Zitto amesema ili sauti za walemavu zisikilizwe kikamilifu ni lazima uteuzi uzingatie walemavu wenyewe na kuwa ni vyema serikali ikahakikisha kuwa walemavu wanakuwa na wawakilisha katika ngazi ya mabaraza ya madiwani.