Prof. Sospeter Muhongo - Waziri wa Nishati na Madini
Waziri Muhongo pia ameahidi kuendeleza mradi wa usambazaji umeme vijijini ili kutimiza lengo la kila mtanzania kuwa na uhakika wa kupata nishati ya umeme.
Profesa Muhongo amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kikanda wa masuala ya nishati endelevu uliwakutanisha washiriki kutoka nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Afrika.
Katika mkutano huo, Waziri Muhongo amewataka wadau hao kutafuta suluhisho la upungufu wa nishati kwa kuzingatia malengo ya milenia yanayotaja nishati kama moja ya sababu za kuinua uchumi.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez amesema nchi za Afrika zinahitaji kutumia teknolojia, sera na uwezo walio nao katika kupambana na suala la upungufu wa nishati huku umoja huo ukiahidi kutumia jumla ya dola za Kimarekani bilioni mbili katika kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu.





.jpg?itok=5cvL0YaP)