Wednesday , 7th Feb , 2018

Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa mvua kubwa katika baadhi ya mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Ruvuma kuanzia leo usiku.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumatatu) na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa taarifa kamili angalia hapa chini.