Sehemu ya mji wa Dodoma
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, mtaalamu wa Jiolojia mkoa wa Dodoma, Gabriel Mbogoma amesema kuwa tetemeko hilo limetokea majira ya saa 12:02 asubuhi na lilidumu kwa muda wa sekunde thelathini tuu na hivyo kuzua taharuki kwa watu.
Amesema tetemeko hilo lilianzia katika kijiji cha Haneti kilichopo Wilayani Chamwino Mkoani hapa na kutikisa katika mikoa ya Arusha, Tanga na Dar es Salaam.
Hata hivyo amesema hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa kufuatia tetemeko hilo lililoelezwa kuwa ni la pili kwa ukubwa tangu lile lililotokea mwaka 2007 ambalo lilianzia katika milima wa Oldonyolengai Mkoani Arusha lililokuwa na ukubwa wa kipimo cha Ritcher 5.9






