
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma, Faustine Mwakalinga
Wito huo umetolewa leo na mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma, Faustine Mwakalinga wakati akizungumza na East Afrika Radio kuhusiana na faida za wiki ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara nchini.
Mwakalinga amesema kuwa elimu inayotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuhusiana na umuhimu wa kulipa kodi ina faida kubwa kwa wafanyabiashara hata kwa wale ambao wanakwepa kulipa kodi kwani wakipata elimu ya kutosha wanaweza kuanza kulipa kodi kwa ajili kukuza uchumi wa Taifa.
Pia ametoa wito kwa Jumuiya za wafanyabiashara kuhakikisha kuwa zinatatua matatizo yao na serikali kwa kukaa mezani na kuachana na migomo isiyokuwa na tija kwa taifa.