Monday , 22nd Jun , 2015

Shirika la viwango Tanzania TBS limesema kuwa limeingia mkataba na Ofisi ya Waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa kudhibiti bidhaa hafifu na bandia.

Bidhaa hafifu zikiwa dampo tayari kabisa kwa kuteketezwa.

Afisa masoko wa TBS Gladness Kaseka amesema ili kufanikisha ushirikiano huo wameanza kutunga sheria zitakazowasaidia kuwaongoza Tamisemi kufanya kazi kwa weledi hivyo ni vyema wafanyabishara wakazalisha bidhaa bora.

Aidha Bi. Gladness ameongeza kuwa jamii isikubali kununua bidhaa zisizo thibitishwa na shirika hilo na kusema kuwa vita dhidi ya bidhaa hafifu itafanikiwa iwapo jamii itashiriki moja kwa moja.

Amesema kuwa ili kuhakikisha bidhaa hafifu zinadhibitiwa wameanza mpango wa kufungua ofisi za kanda mipakani na kwenye viwanja vya ndege ambapo tayari washafungua ofisi hizo Mbeya, Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.