
Waziri wa Katiba na Sheria wa Dkt. Harison Mwakyembe
Masharti hayo ni pamoja na kuwaruhusu wananchi na taasisi za kiraia kufikisha malalamiko yao ili kuimarisha demokrasia na utawala bora.
Wito huo umetolewa jana mkoani Arusha na Waziri wa Katiba na Sheria wa Dkt. Harison Mwakyembe alipokuwa anafungua kongamano la kimataifa lililohudhuriwa na washiriki zaidi ya 150 kutoka taasisi mbalimbali zinazosimamia haki za binadamu katika nchi za Umoja wa Afrika.
Dkt. Mwakyembe alisema pamoja na umuhimu wa mahakama hiyo katika kudumisha haki za binadamu kati ya nchi 54 wanachama wa (AU) ni nchi 30 pekee zilizoridhia itifaki ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo na kati ya hizo ni nchi nane tu zilizotoa tamko la kuwaruhusu wananchi na taasisi za kiraia kufikisha malalamiko yao kwenye mahakama hiyo.
Kwa upande wake rais wa mahakama ya Africa aliyemaliza muda wake Jaji Agustino Ramadhani wamesema kukosekana kwa utashi wa kisiasa miongoni mwa nchi wanachama wa (AU) ni baadhi ya sababu zinazochangia nchi nyingi kushindwa kutekeleza makubaliano waliyojiewekea.