Friday , 11th Jul , 2014

Serikali ya Tanzania imeiomba serikali ya uingereza kulirudisha shirika la ndege la British Airways ili lianze tena safari zake hapa nchini ili kusaidia kukuza biashara na utalii.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Kamilius Membe.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Bernad Membe amesema tayari wameshawasilisha maombi hayo kwa serikali ya Uingereza.

Shirika hili liliacha kufanya kufanya safari zake za moja kwa moja kati ya Tanzania na Uingereza mwezi machi mwaka jana likieleza kuwa lilikua likiendesha shughuli zeke hizo kwa hasara.

Membe amesema Tanzania imeshakua kiuwekezaji na kwamba shirika hilo likirudisha huduma zake wigo wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili utapanuka.

Wakati huo huo, taasisi zinazotoa mikopo na uwezeshaji kwa wanawake zimetakiwa kufikiri namna ya kutoe elimu ya ujasiriamali ili mikopo wanayotoa ilete tija kwa wajasiriamali hao.

Mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa Arusha Bi. Catherine Magige amesema hayo wakati akikabidhi msaada wa fedha kwa vikundi vya kina mama na kuongeza kuwa wanawake wengi wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu ujasiriamali .

Nao baadhi ya wakinamama wasema kupitia elimu ya ujasiamali waliyoipataa kupitia taasisi ya mbunge huyo,itawasaidi katika kufikia malengo yao hasa katika kupanga mapato na matumizi ya fedha wanazo kopeshwa.

pesa taslimu shilingi milioni moja na vifaa vyenye gharama shilingi milioni tatu vimekabidhiwa kwa wakinamama hao lengo likiwa kuwawezesha wakinamama wajasiliamali kuweza kujiendeleza kiuchumi.