Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania,Badra Masoud
Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud, ugunduzi huu wa gesi una thamani ya takribani shilingi za Tanzania trillioni 12 sawa na takribani dola za Kimarekani bilioni 6.
Msemaji huyo wa Wizara ya Nishati amesema kuwa utafiti kuhusu gesi hii umedumu kwa takribani miaka hamsini ukihusisha makampuni mbalimbali.
Aidha Masoud amesema uvunaji wa gesi hii utaanza muda wowote mara tu baada ya kukamilika kwa miundombinu ambapo gesi nyingine itauzwa nje na nyingine itaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Tanzania bado inaamini huenda kuna gesi zaidi itagundulika kwa kuwa utafiti zaidi bado unaendelea.