Friday , 7th Mar , 2014

Tanzania inakabiliwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa hatari wa homa ya ini, ambapo kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo hivi sasa ni mara kumi ya yale ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kampeni ya kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kujikinga dhidi ya ugonjwa huo, ambao maambukizi yake yanafanana kabisa na yale ya virusi vya Ukimwi.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa kuna haja kwa jamii kuacha tabia na vitendo hatarishi zikiwemo ngono zembe, sambamba na kwenda kupima iwapo mtu ana ugonjwa huo, na kupata chanjo kwa watoto wadogo ambao bado hawajaambukizwa ugonjwa huo.