Wednesday , 26th Sep , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hakuwahi kusaidiwa na mtu yeyote mpaka kuwa kiongozi kwa nyadhifa mbalimbali za kisiasa nchini katika nafasi alizozihudumia akiwa kama Mkuu wa Wilaya na badae Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mrisho Gambo ameandika kwa kumbukumbu yeye na wazazi wake walikuwa watu wa hali ya chini lakini alipigana mpaka kufikia mafanikio aliyonayo sasa.

Marehemu Mama yangu (ambaye ndiye alikuwa nguzo yangu) alikuwa muuza uji Mchikichini Ilala na baba yangu dalali wa ndizi sokoni Kariakoo. Sina ndugu yoyote kiongozi wala sina God Father, nimeingia kwenye masuala ya uongozi kwa kudra zake Mungu.” Aliandika Mrisho Gambo

Ninazungumza na wewe uliyekata tamaa kwa kuwa toka umalize chuo hujapata kazi, au unafanya biashara lakini hujafanikiwa. Maisha ni milima na mabonde, ukiona unakaribia kukata tamaa kwenye maisha jua mafanikio yapo karibu.” Aliongeza Mrisho Gambo