Thursday , 18th Jun , 2015

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesemaimewatoa hofu watanzania kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi ambapo imesema kuwa thamani ya shilingi itaimarika ndani ya muda mfupi ujao

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema imeshanza kuchukua hatua zitakazosaidia kuimarisha shilingi ya Tanzania ili isiendelee kuporomoka zaidi dhidi ya dola ya Marekani na kuhakikisha kwamba uchumi wa nchi unaendelea kuimarika.

Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania Bw. Lusajo Mwankemwa ameaimbia Hot Mix leo jijini Dar es Salaam kwamba BOT ina akiba ya kutosha ya matumizi ya fedha za kigeni ikiwemo dola.

Bw. Mwankemwa amesema hakuna haja kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuwa na hofu kwa kuwa tayari BOT ina akiba ya dola za Marekani kwa matumizi ya nchi nzima kwa kipindi cha miezi minne hata kama itakuwa hazingii nchini.

Watanzania wametakiwa kutokuamini maneno yanayoenezwa juu ya kupotea kwa shilingi mia tano ya sarafu katika maeneo kadhaa ya nchi kuwa kuna uhusiano na pesa hiyo kununuliwa ili kutengeneza vidani vya shaba.

Afisa wa huduma za kibenki wa Benki Kuu ya Tanzania Patrick Fata amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi wa kuwepo kwa tetesi za pesa hiyo kutumika nchini kwa kuyeyushwa na kutengeneza vidani vya shaba..