Friday , 8th Aug , 2014

Tanzania leo inaadhimisha kilele cha maonyesho ya wakulima na wafugaji nane nane ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza.

Maonyesho hayo ambayo mwaka huu yamegawanywa kikanda kwa bidhaa tofauti ikiwa Nyanda za juu kusini yatafanyika jijini Mbeya ambapo yatakua maalumu kwa kilimo wakati Kanda ya kaskazini yatafanyika Dodoma ambapo itakua maalumu kwa mifugo na Lindi ndipo yatapofanyika maadhimisho ya Kitaifa.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka wizara ya kilimo na chakula imesema lengo la kufanya maonyesho hayo Kikanda ni kuweza kutoa fursa kwa eneo husika kulingana shughuli inayofanyika katika kanda hiyo kwa kiasi kikubwa.