Thursday , 27th Oct , 2016

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha amesema ili Tanzania iweze kunufaika na mifugo iliyonayo ni lazima wadau wote wa sekta hiyo wabadilike na kufuga kisasa.

Mifugo (ng;ombe) wanaofugwa kienyeji

Ole Nasha ametoa kauli hiyo jijini Arusha, baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa chama cha wataalam wa uzalishaji wa mifugo ambapo amesema kuwa asilimia 97 ya wafugaji nchini wanafuga ufugaji wa asili usio na uwezo wa kutoa matokeo ya uchumi unaokusidiwa kulinganisha na mifugo iliyopo nchini.

Naibu Waziri huyo amesema wafugaji wengi hawajaweza kukuza mifugo yao kwa ajili ya mahitaji ya soko hali inayowafanya kuwawia vigumu kuweza kupata soko la kimataifa na kuondoa umasikini kupitia mifugo yao kupitia uuzaji wa nyama, ngozi na maziwa.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mifugo na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Annesiata Njombe, amesema Tanzania huuza wastani wa tani elfu moja za nyama kwa mwaka na kuwa endapo mifugo itaboreshwa kutakuwa na soko kubwa la bidhaa za mifugo.