Thursday , 14th Jul , 2016

Serikali imetangaza katika eneo la Mkiu katika wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kuwa eneo maalumu la ujenzi wa viwanda vya kuzalishia bidhaa zinazouzwa nje ya nchi(EPZA).

Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage

Uamuzi huo umetolewa na Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage baada ya waziri Mkuu kutembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza marumaru kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

Mhe Mwijage amesema kuwa balozi wa China alikubali kuleta wawekezaji nchini wa kujenga viwanda endapo atapatiwa eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa viwanda mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka wizara hiyo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha kuwa wanaunganisha eneo hilo na bomba la gesi na kutengeneza mtambo wa kufua umeme ili kuendesha shughuli hizo za viwanda.

Sauti ya Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage