Thursday , 30th Apr , 2015

Wakulima wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wameiomba serikali kutazama namna ya kurahisisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima wadogo ili kuinua kilimo na uchumi wa wakulima hao na kuwafanya kushiriki katika ukuzaji wa uchumi wa taifa.

Meneja masoko wa kampuni ya usambazaji mbegu za mazao mbalimbali ya Suba agro, Hamza Msuya.

Mmoja wa wakulima kutoka katika kijiji cha Iulahumba kata ya Mdandu wilayani humo Bw, Anthon Mfilinge amesema uwezo wa wakulima wadogo kujitegemea bado ni changamoto.

Anthony ameongeza kuwa ni muhimu serikali iwe na mipango thabiti ya kusaidia wakulima kwa kuweka utaratibu mzuri unaofahamika vema na pia kufikisha pembejeo hizo kwa wakati.

Meneja masoko wa kampuni ya usambazaji mbegu za mazao mbalimbali ya Suba Agro, Hamza Msuya amesema ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua kilimo makampuni yanayosambaza pembejeo ni vema yakawasaidia wakulima kwa kuwatembelea mara kwa mara ili kuona changamoto zao na kuona namna ya kuzitatua.

Kwa upande wao wadau wengine wa kilimo wamesema kuwa ni vema serikali ikamaliza changamoto za upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima ili kukifanya kilimo kuwa moja ya sekta za kukuza uchumi wa nchi.