Makamu wa rais nchini Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhasibu mwandamizi kutoka benki kuu ya Tanzania kitengo cha Bima ya Amana, Balthazar Laurent, kwenye maonyesho ya wakulima na wafugaji Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma.
Laurent amesema kila taasisi ya kifedha ambayo inajiendesha hapa nchini imejisajili kwenye bima ya Amana iliyopo chini ya usimamizi wa Benki Kuu na hivyo kumlinda mteja pindi taasisi husika ya kifedha inapofilisika.
Kwa upande wake Meneja wa Benki Kuu ya Tanzania Kanda ya kati, Harry Mwansembo, amesema kuwa bima hiyo ya amana haihusiani na majanga ya moto au ya wizi yanayotokea benki, kwa kuwa majanga hayo yana bima nyingine ambazo zinaweza kuyashughulikia.
Katika hatua nyingine, serikali imefanya marekebisho makubwa kwenye vyama vya ushirika baada ya kuonekana kuwa na uongozi mbovu pamoja na ubadhirifu wa fedha kiasi ambacho wakulima kuona hakuna faida ya kujiunga na ushirika.
Akiongea katika maadhimisho ya siku ya wakulima nane nane yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo Makamu wa Rais wa Tanzania Dk.Ghrib bilal amesema kuwa serikali imeshatunga sheria mbalimbali za kuweza kuimairisha ili kuleta tija kwa wakulima
Dk.Bilal amesema kuwa vyama vya ushirika ndio vinatakiwa kuwa nguzo ya wakulima ambapo itaweza kuwasaidia kuweza kupata soko ndani na nje ya nchi na kuondoa umasikini nchini na kufikia malengo ya kauli mbiu ya mwaka huu kilimo ni biashara kwa matokeo makubwa sasa.