Kampuni hiyo yenye makao yake makuu Thika, nchini Kenya itanunua tani laki moja za Korosho ghafi zenye thamani ya shilingi 418 bilioni.
Waziri wa viwanda na biashara Joseph Kakunda amesema serikali inaendelea kuwakaribisha wanunuzi wa Korosho kutoka nje ya Tanzania kwa maslahi ya uchumi wa taifa na mkulima.
Mbali na uwepo wa Waziri Kakunda, Makubaliano hayo yameshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Dkt. Hussein Mansour na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Indopower Solution, Brian Mutembei.





