
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Akizungumza leo kwenye maadhimisho ya kuchangia damu salama yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Nyerere Square Mwalimu alisema kuwa tabia ya waganga Wakuu wa Hospitali za Wilaya na Mikoa kuwauzia damu wagonjwa ndio chanzo kikubwa kunachopelekea wananchi kutokuwa na moyo wa kuchangia damu.
Ametoa wito kwa waganga wote waliopo kwenye vituo vya afya vya serikali na hospitali zote za mikoa nchini kuweka mabango yanayoelezea kuwa damu haiuzwi bali inatolewa bure.
Kwa upande wake meneja wa mpango wa damu salama nchini, Dk, Abdul Juma amesema kuwa taifa bado lina changamoto kubwa ya uhaba wa damu salama hali inayohatarisha uhai wa watoto wadogo, akina mama wajawazito na majeruhi wa ajali mbalimbali.