Friday , 7th Aug , 2015

Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa wa kuwapatia ruzuku wachimbaji wa madini wadogowadogo hapa nchini ,ili kuwawezesha kufanyaka kazi ya uchimbaji kwa utaalamu na kuacha kuwa tegemezi kwa kuingia mikataba na wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wakitafuta madini kwa kutumia mfumo ambayo ni dunia

Wachimbaji hao wametoa kilio kwa Mkuu wa wilaya hiyo Bw, Fadhili Mkuru kukagua machimbo hayo ambayo yapo wilayani Mkalama, wamesema kutokana na wao kutokuwa na dhana za uchimbaji ina walazimu kuingia ubia kwa kugawana kwa asilimia 70 kwa 30 na wawekezaji na wao kuchukuwa udongo wote wakopa na kwenda kuchujia nje ya nchi.

Akijibu malalamiko ya wachimbaji hao kaimu kamishina msaidizi wa madini kanda ya kati Muhandisi Gabriel Senge amewatoa wasiwasi wachimbaji hao kwa sababu ofisi yake imesha peleka mapendekezo ya kuwaombea wachimbaji wadogo wa madini ya kopa kupatiwa ruzuku ya dola laki moja,ambazo zita wasidia kupata mitambo na kufanya utafiti wa madini kwa njia ya kisasa tofauti na sasahivi wanachimba kwa hisia.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mkalama Bw, Fadhili Nkuru baada ya kufanya ukaguzi na kusikiliza malalamiko ya wachimbaji ,amewaagiza kutoa mara moja malundo ya udongo ambayo yame kuwa tishio kwa binadamu na wanyama kufukiwa hasa kipindi cha mvua kitakapoanza