Friday , 25th Nov , 2016

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema takribani asilimia 27 katika vifo vinavyotokea nchini vinasabishwa na magonjwa yasiyoambukizwa.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Mhe. Ummy ametoa takwimu hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati akipokea vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 300 kutoka kwa wadau wa afya nchini na kuongeza kuwa changamoto kubwa ambayo kwa sasa serikali imewekea kipaumbele ni kufanya huduma za uchunguzi hasa kwa yale magonjwa yasiyoambukizwa.

Waziri Mwalimu amekiri serikali haifanyi vizuri katika huduma za macho nchini hivyo ni wajibu kwa wadau wa maendeleo kujitokeza zaidi.

Kwa upande wake muwakilishi wa Wadau hao wa maendeleo nchini Bw. Sanjay Rughani amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kwa lengo la kuwasaidia watanzania wa hali ya chini ambao hawana uwezo wa kufikiwa na huduma hizo kwa wakati.