Thursday , 14th Jul , 2016

Wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imekanusha taarifa inayodai kuwa serikali imepanga kushusha mishahara ya madaktari kwa asilimia 30 sambamba na kufuta posho za wataalamu wa afya walio katika mafunzo kwa vitendo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kitengo cha mawasiliano kutoka wizara ya afya imeeleza kuwa kumekuwepo na upotoshaji juu ya taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa wizara hiyo juu ya kufutwa kwa kibali cha msajili wa hazina kwa utoaji mishahara kwa watumishi wa hosptali ya bugando.

Wizara ya afya imeeleza kuwa, Hosptali ya Bugando sio shirika la umma hivyo walistahili kulipwa mishahara kama watumishi wengine na si kweli kuwa kiwango cha mishahara kitapunguzwa na uamuzi huo wa Msajili wa Hazina utaihusu Hospitali ya Bugando pekee.

Aidha, serikali aijafuta posho kwa wanajifunza kwa vitendo na suala la ajira litashugulikia mara baada ya zoezi la uhakiki kukamilika ambapo wananchi na watumishi wa sekta ya afya kupuuzia uvumi huo wenye lengo la kupotosha umma